CELTIC WADHIBITISHA UHAMISHO WA KIBET
Hali tata kuhusu mustakabali wa nyota wa Kenya wa U-20, Aldrine Kibet hatimaye zimepata jibu baada ya klabu ya ligi kuu ya Uhispania RC Celta Vigo kuthibitisha rasmi uhamisho wake kwa kandarasi ya miaka minne itakayotumika hadi 2029.
Tangazo hilo lilitolewa kwenye kurasa rasmi za kilabu, na kueleza kwamba Kibet anajiunga na Celta Fortuna, timu B, na atasajiliwa kama mchezaji chipukizi mwenye nfsi ya kujumuishwa taratibu katika kikosi cha wakubwa. Taarifa hiyo ilisifu kasi yake, ustadi wa mpira, na ubora wa ufungaji, sifa ambazo zilivutia hisia za kimataifa wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika U-20.
Safari ya soka ya Kibet ilianza katika Shule ya Upili ya Wavulana ya St. Anthony’s mjini Kitale, ambapo aliongoza timu hiyo hadi kutwaa ubingwa wa kitaifa 2023. Alitajwa kuwa MVP na mfungaji bora, akiwa na mabao 25 na asisti 27, uchezaji bora ambao ulimtambulisha kama mmoja wa nyota ibuka wa Kenya.
Baada ya shindano hilo, na chini ya mpango wa Talanta Hela uliozinduliwa na Waziri wa Michezo wa wakati huo Ababu Namwamba, Kibet alihamia Nastic Sports Academy nchini Uhispania, ambayo iliweka msingi wa hatua hii kuu ya taaluma yake.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































