VUTA VUTA ZA SHA ZAINGIA SIASA
Madai kwamba hospitali kadhaa zimekuwa zikiilaghai mamlaka ya SHA kwa kuitisha malipo kwa huduma ambazo hazikutolewa yamechukua mkondo wa kisiasa, waziri wa afya Aden Duale akidai kwamba baadhi ya hospitali zilizogunduliwa na kufungwa zinamilikiwa na baadhi ya wabunge.
Kauli za waziri huyo zimejiri baada ya wabunge hao kumtaka ajiuzulu kutokana na madai kwamba SHA imekuwa ikitoa malipo kwa hospitali hewa, madai ambayo Duale kuwa juhudi za kulemaza vita dhidi ya ufisadi katika sekta ya afya.
Wakizungumza wakati wa vikao vya bunge, wabunge walio chini ya vuguvugu la Kenya Mpya wameshinikiza kuwa ni sharti Duale awajibishwe.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































