MACHAKOS YASISITIZA HUDUMA ZINGALIPO
Serikali ya kaunti ya Machakos imekiri kutatizika kwa huduma za matibabu katika hospitali za umma kutokana na mgomo wa wauguzi ambao unaingia siku ya 7, ila ikasisitiza kuwa masuala yaliyoibuliwa na wauguzi yanazikabili kaunti zote nchini.
Katika kikao na wanahabari, katibu wa kaunti hiyo Muia Ndambuki, amepuzilia mbali ripoti kuhusu kulemazwa kwa huduma zote za matibabu kwenye kaunti hiyo, na kushikilia kuwa baadhi ya huduma zinaendelea kutolewa.
Aidha, amesema mazungumzo yameanzishwa na muungano wa wauguzi KNUN.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































