MVURYA AWARAI WAKENYA KUUNGA MKONO HARAMBE STARS
Waziri wa Michezo Salim Mvurya amewataka Wakenya kuunga mkono Harambee Stars kabla ya Michuano ya Mataifa ya Afrika ya 2024-CHAN- itakayoanza Agosti 2 hadi Agosti 30, 2025.
Akizungumza wakati wa makabidhiano rasmi ya Uwanja wa Nyayo na viwanja viwili vya mazoezi, Police Sacco na Ulinzi Complex kwa Kamati ya andalizi, Mvurya alisema Kenya iko katika hatua ya mwisho ya maandalizi.
Mvurya aliitaja CHAN kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi, na amewahakikishia mashabiki bei nafuu ya tiketi kuanzia shilingi 200 hadi 1,000.
Pia alikuwepo Waziri wa Ulinzi Soipan Tuya, ambaye aliwataka mashabiki kuheshimu miundombinu ya uwanja na kuepuka uharibifu wakati wa kusherehe timu zao.
Huku mguso wa mwisho ukiendelea, macho yote sasa yako kwa Harambee Stars kung’ara nyumbani.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































