RUTO AFICHUA AFISA ALIFARIKI HAITI
Familia ya afisa wa polisi Bernard Kabiru aliyeripotiwa kutoweka mwezi Machi nchini Haiti inashinikiza serikali kuweka wazi kilichomfanyikia mwanao, kutokana na kauli ya Rais William Ruto hapo jana kwamba afisa huyo alifariki.
Akizungumza katika kikao cha kujadili hali ya usalama nchini Haiti, akiwa jijini New York Marekani, Ruto aliwaomboleza maafisa 3 waliofariki akiwemo Kabiru, ambaye muda wote idara ya polisi humu nchini imekuwa ikiiambia familia yake kwamba anasakwa.
Familia hiyo sasa imeelekea mahakamani ikitaka amri itolewe kuishinikiza serikali kutoa majibu kwa maswali yao mbali na mwili wa jamaa yao kurejeshwa nchini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































