#Local News

USHIRIKIANO WA ODM-UDA HAUPO, SIFUNA ADAI

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna ametangaza kuwa makubaliano ya ushirikiano baina ya chama hicho na UDA hayapo tena, akisema makubaliano hayo yalivunjika rasmi wakati wa mauaji ya bloga Albert Ojwang mikononi mwa maafisa wa polisi.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini, Sifuna amesema kuwa makubaliano hayo yalilenga kulinda maisha na demokrasia nchini.

Aidha, amelalamikia madai kwamba UDA haina nia njema ya kushirikiana na kinara wa ODM Raila Odinga.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *