#Business

JIANDAENI KWA MEZA KAVU, WAKENYA WAONYWA

Wakenya sasa watalazimika kujizatiti kununua vyakula kwa bei ya juu

katika siku za hivi karibuni kutokana na mfumuko wa bei ya vyakula na mifumo mibaya ya hali ya hewa.

Katika ripoti yake ya hivi punde kwa kamati bajeti, afisi ya inayosimamia bajeti bungeni imebashiri kipindi cha mvua iliyo chini ya wastani
inayotarajiwa kuanzia mwezi wa Oktoba hadi Desemba  mwaka wa 2025, hali inayotarajiwa kuathiri uzalishaji wa  mboga na  vyakula vinginevyo.


Kati ya mwezi wa Juni 2024 hadi Agosti 2025, bei ya vyakula muhimu ikiwemo mboga, mafuta ya kupikia na sukari ilirekodiwa kuongezeka.


Hata hivyo, ripoti hiyo imeangazia kushushwa kwa bei ya mafuta  huku bei hiyo katika soko la kimataifa ikiratibiwa kupanda.

Katika kipindi cha mapito ,bei ya mafuta taa ilishuka kwa 9.7%, diseli
5.7% na petroli ikashuka kwa  6.4%.
Hata hivyo, ripoti hiyo imeoonya kwamba  mvutano wa kijiografia na
kisiasa hasa katika maeneo ya  Mashariki ya kati  inaendelea
kuhatarisha  soko la  nishati.
Sekta kama vile nguo na viatu, afya , migahawa  na malazi  pia
ilishuhudia kuongezeka kwa bei.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

JIANDAENI KWA MEZA KAVU, WAKENYA WAONYWA

USALAMA KWENYE FOLENI

JIANDAENI KWA MEZA KAVU, WAKENYA WAONYWA

14 WAKAMATWA KITALE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *