#Sports

WANARIADHA WA KENYA WATIA FORA WAC

Wakenya walitia fora na kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Marekani kwenye mashindano dunia ya ubingwa wa riadha duniani yaliyokamilika hapo jana jijini Tokyo nchini Japan.

Kenya ilipata jumla ya medali 11, zikiwemo dhahabu 7, fedha 2 sawa na shaba, nyuma ya Marekani waliojizolea jumla ya medal 26.

Wakenya waliopata dhahabu ni Beatrice Chebet katika mbio za mita 10,000 na mita 5,000, Peres Jepchirchir katika mbio za marathon, Faith Kipyegon katika mbio za mita 1,500, Faith Cherotich kwenye mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji, Emmanuel Wanyonyi na Lilian Odira katika mbio za mita 800 kwa wanaume na wanawake mtawalia.

Imetayarishwa na Nelson Andati

WANARIADHA WA KENYA WATIA FORA WAC

WAGONJWA WALIOPONA WAZUILIWA MTRH

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *