USALAMA KUIMARIKA KERIO VALLEY
Juhudi za serikali za kurejesha utulivu katika eneo la Kerio Valley zimeendelea kuzaa matunda, baada ya jamaa mmoja aliyekiri kuwa mhalifu sugu kujisalimisha kwa polisi akitangaza kwamba ameasi Maisha ya uhalifu.
Mwanaume huyo, kwa jina la Arthur Komen mwenye umri wa miaka
30, alijiwasilisha katika kituo cha polisi cha Tot kaunti ya Elgeyo Marakwet alikopeana bunduki na risasi kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi wa kidini kwa ushauri nasaha.
Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Kerio Valley, Zablon Okyo
alihibitisha tukio hilo na kusema kuwa ni hatua kubwa ya kuleta
amani katika eneo hilo tete.
Akiwa kwenye kituo hicho, Komen ameahidi kuwasalimisha wenzake ambao wangali mafichoni mbali na kuwa balozi wa amani.
Naibu wa Kamanda Ezekiel Amonde amekaribisha hatua hiyo na kuwarai
washukiwa wengine kufuata nyayo za Komen akisema kwamba, huku wakaazi wakiwa na
matumaini kwamba huo ndio mwanzo wa uponaji na utulivu katika eneo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































