MACARTHY AWATEMA WACHEZAJI WATANO
Kocha wa Harambee Stars Benni MCarthy amewatema wachezaji watano kwenye kikosi chake kuelekea michuano ya CHAN.
Wachezaji waliotemwa ni; Yakeen Muteheli na Staphod Odhiambo wa Ulinzi Stars, Keith Imbali wa Shabana, Kelly Madada wa AFC Leopards na kipa wa Tusker FC Brian Opondo.
Kocha huyo alieleza ugumu wa uamuzi wake kuzima ndoto za wachezaji hao lakini akasema anatakiwa kufanya maamuzi kwa maslahi ya taifa ambayo yanaambatana na maamuzi hayo magumu.
Alieleza zaidi kuwa kutemwa kwa wachezaji hao hakutokani na kutokuwa na ubora bali ni lazima atafute kikosi bora cha nchi.
Timu hiyo ilijumuika katika mazoezi yao na Rais William Ruto, aliyewatembelea akiandamana na Waziri wa Michezo Salim Mvurya, na mwenzake wa Ulinzi Soipan Tuya.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































