#Local News

NPS YAENDELEZA AFYA YA KIAKILI

Idara ya huduma za polisi NPS imeanzisha juhudi za kuimarisha afya ya kiakili ya maafisa wake kupitia mafunzo yanayotolewa kwa washikadau wakwemo wataalam wa ushauri nasaha na wanasaikolojia ambao hushughulikia afya ya kiakili ya maafisa hao.

Mafunzo hayo ya siku 4, yanatolewa kwa ushirikiano na shirika la International Justice of Kenya, yakiwalenga watu 43 walio na jukumu la kutoa
msaada kwa maafisa wa polisi ambao wenye matatizo ya afya ya kiakili
na hata familia zao.


Naibu Inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat, amesisitiza  kuwa maafisa wa polisi
huwa mstari wa mbele katika ulinzi wa wananchi, akikariri kuwa kuna haja ya kuhakikisha kuwa maafisa  hao wanasalia imara kiakili.


Hata hivyo,Lagat amewakikishia kuwa wataungwa mkono
kikamilifu kupitia uwezeshaji wa waelekezi wa ushauri nasaha, ambao
utawasaidia kiroho, kihisia na kisaikolojia ili kuiimarisha afya
yao ya kiakili 

Kulingana na ripoti ya IPOA, visa 57 vya maafisa wa polisi kujiua vlirekodiwa kati ya mwaka wa 2016 na 2020, huku , maafisa 65 wakwaiua raia ambao wanaaminika kuwa wapenzi wao, familia, marafiki na hata wale wanaofanya kazi pamoja na wao.

Imetayarishwa na Antony Ngongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *