STARS WACHEZA NA SHARKS KAMA MAANDALIZI YA CHAN
Harambee Stars ilianza maandalizi yake ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 kwa taabu kufuatia kufungwa 2-1 na Timu ya Sharks Family katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Kasarani Annex Grounds.
Timu ya Sharks Family, inayojumuisha wachezaji wa zamani wa Kariobangi Sharks, ilipata mabao yake kupitia kwa Eli Asieche na Shaphan Oyugi huku Bao pekee la timu ya taifa lilipatikana katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Austine Odhiambo.
Stars, ilicheza vipindi vitatu, vilivyomalizika kwa ushindi wa bao 1-0, sare ya 0-0 na kufungwa 2-0.
Kampeni ya Kenya katika CHAN inaanza dhidi ya DR Congo Jumapili, 3 Agosti, kabla ya kukabiliana na Angola (Alhamisi, 7 Agosti), Morocco (Jumapili, 10 Agosti), na Zambia (Jumapili, 17 Agosti).
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































