KARO VYUONI YAPUNGUZWA
Ni afueni kwa wanafunzi wanaosomea kozi mbali mbali kama vile udaktari na usanifu ujenzi baada ya serikali kutangaza kupunguzwa kwa karo wanayolipa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.
Hatua ya wizara ya elimu kupunguza karo kwa baadhi ya kozi katika vyuo vikuu vya umma imechukuliwa kufuatia mapendekezo ya kamati maalum ya elimu iliyoteuliwa na rais William Ruto mwaka jana.
Aidha, ufadhili na mikopo ya serikali itaendelea kutolewa kwa wanafunzi katika vyuo vikuu vya umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































