DCI YAKANA ‘KUIBA’ DETA ZA WAKENYA
Idara ya upelelezi wa jinai DCI imepuzilia mbali taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti moja nchini hii leo zikidai kwamba idara hiyo inatumia program maalum kupata deta za siri kwenye simu za wakenya.
Kwenye taarifa, gazeti hilo limedai kwamba DCI iliweka program hiyo inayofahamika kama FlexiSpy kwenye simu za watengenezaji wa Makala ya Blood Parliament ya shirika la habari la Uingereza BBC, muda mfupi baada ya kuwakamata.
Hata hivyo, DCI imezitaja taarifa hizo kuwa za uongo, ingawa haijaweka wazi maelezo kuhusu madai hayo, kwa misingi kwamba suala hilo linaendelea mahakamani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































