#Sports

GYOKERES ANYIMWA NDOTO YA JEZI NAMBARI TISA

Hatimaye Viktor Gyokeres yuko mbioni kujiunga na Arsenal baada ya The Gunners kufanikiwa katika mazungumzo na Sporting Lisbon, na kukubali kulipa jumla ya pauni milioni 63.7 baada ya kuhangaika kuhusu nyongeza .

Ata hivyo Arsenal haitaweza kumpa Viktor Gyokeres jezi ya ndoto yake ya nambari tisa wakati mshambuliaji huyo wa Uswidi atakapokamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 63.7 kwenda Emirates.

Gyokeres, 27, amedhamiria kujiunga na The Gunners katika kipindi chote cha uhamisho wa majira ya kiangazi na yuko mbioni kupata matakwa yake.

Masharti ya kibinafsi yamekubaliwa kwa muda mrefu lakini maelezo ya kina ya makubaliano kati ya Arsenal na Sporting Lisbon yalichukua wiki kadhaa kukamilika.

Mabingwa hao wa Ureno, ambao Gyokeres amefunga mabao 97 katika mechi 102 mbali, walikuwa wakihangaika juu ya asili ya nyongeza ambayo ilikuwa sehemu ya ofa ya Arsenal.

Gyokeres amevalia jezi namba 9 tangu ajiunge na Sporting akitokea Coventry mwaka 2023.

Jezi hiyo katika kikosi cha Arsenal ni ya Gabriel Jesus, ambaye amekuwa nje ya uwanja hadi majira ya joto kufatia majeruhi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

GYOKERES ANYIMWA NDOTO YA JEZI NAMBARI TISA

ODERA APIGIA UPATO MZUNGUKO WA RAGA

GYOKERES ANYIMWA NDOTO YA JEZI NAMBARI TISA

WANARIADHA WAWILI WAPIGWA MARUFUKU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *