IDARA YA UTABIRI YATANGAZA WIKI YA MVUA
Wakenya wametahadharishwa kuhusu uwezekano wa mvua kubwa wiki hii, wakitakiwa kujiandaa ili kuwa salama.
Katika utabiri wake wa hivi punde, idara ya utabiri wa hali anga imesema huenda wiki hii ikashuhudia vipindi vya mvua, anga yenye mawingu mazito na joto kali majira ya mchana na usiku wa bairidi.
Katika kipindi cha kati ya tarehe 2 hadi 8, maeneo ya Ziwa Victoria, Magharibi, nyanda za juu za kati na pwani yataendelea kushuhudia mvua, ambayo huenda ikaathiri usafiri na ukulima.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































