#Local News

SHA YAMULIKWA KUHUSU UAJIRI WAKE

Washikadau mbali mbali wameendelea kushinikiza uchunguzi huru kufanywa katika Sakata ya ajira kwenye mamlaka ya afya ya jamii SHA baada ya ripoti kuibuka kwamba mhasibu Andrew Rotich aliyefichua ulaghai wa mamilioni ya pesa ameachwa nje ya orodha ya walioteuliwa upya.

Wa hivi punde ni chama cha wahasibu ICPAK, ambacho kimetaka maelezo kuhusu mchakato wa ajira katika mamlaka hiyo, kikitaka kufahamishwa ni kwanini jina la Rotich liliondolewa kwenye orodha licha ya kuwa bora kwenye mahojiano ya Aprili mwaka huu yaliyomwezesha kuwa naibu mkurugenzi wa ukaguzi.

Rotich ni miongoni mwa wakaguzi waliofichua ulaghai wa mabilioni ya pesa za SHA kupitia bili za matibabu na kusababisha kufungwa kwa hospitali zaidi ya 1,300.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SHA YAMULIKWA KUHUSU UAJIRI WAKE

MAKOMREDI KUANZA MGOMO LEO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *