MAANDALIZI MAZURI YALIVUNIA KENYA USHINDI TOKYO
Makocha wa riadha wamehusisha uchezaji bora wa wanariadha wa kike wa Kenya katika Mashindano ya Dunia ya Riadha yaliyokamilika huko Tokyo Japan na maandalizi mazuri ya kiakili na kimwili.
Wasichana wa Kenya – Faith Kipgeon, Beatrice Chebet, Peris Jepchirchir, Faith Cherotich na Lilian Odora- wote waliambulia dhahabu katika nyanja zao huku Timu ya Kenya ikitoa matokeo mazuri na kutwaa medali 11 kwa jumla na kilele barani Afrika, ikishika nafasi ya pili kwa jumla nyuma ya Marekani.
Kocha mkongwe David Letting, anasema maandalizi mazuri yalikuwa muhimu, katika kukuza vipaji vya wanawake katika mIchezo IjaYo.
Wakati huohuo, Bernard Rono Kalyet, mkufunzi wa mbio za kuruka viunzi Faith Cherotich, pia alizungumzia uchezaji huo, akihusisha ushindi wa wanawake na nidhamu yao, akisema bidii na umakini wao wakati wa mazoezi uliwasukuma kuwashinda wanaume katika michuano hiyo.
Juhudi hizi za pamoja zilihakikisha Kenya inamaliza kama mojawapo ya mataifa bora zaidi Tokyo, kuendeleza utamaduni wa kujivunia wa kuzalisha wanariadha bora wa kike na kuhamasisha kizazi kijacho cha wakimbiaji.
Wachezaji Cole Palmer Kylian Mbappe Achraf Hakimi Raphinha Mohamed SalahVitinha wakibaki kumeza mate tu.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































