#Sports

NYOTA WA RIADHA WAREJEA NA MBWEMBWE

Nyota wa riadha wa Kenya walipata mapokezi ya kishindo Jumanne alasiri waliporejea kutoka kwa Mashindano ya Riadha ya Dunia yaliyomalizika hivi punde jijini Tokyo, Japan.

Wafuasi, maafisa wa serikali na viongozi wa Riadha Kenya walijaa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kusherehekea ushindi wa Timu ya Kenya.

Kenya ilinyakua medali 11 za kuvutia; 7 dhahabu, 2 fedha, na 2 shaba; kushika nafasi ya pili kwa jumla nyuma ya Marekani na kuongoza katika bara la Afrika.

Miongoni mwa wanariadha 48 waliofika ni washindi wanne wa medali za dhahabu: Beatrice Chebet (m 5000, 10000m), Faith Kipyegon (m 1500), Emmanuel Wanyonyi (m 800), na Lillian Odira (m 800).

illian Odira wa Kenya Prisons, ambaye alishangaza ulimwengu kwa kushinda taji la mita 800, alikuwa akishangilia.

Imetayarishwa na Nelson Andati

NYOTA WA RIADHA WAREJEA NA MBWEMBWE

TRUMP: MNAWAZAWADI WANAMGAMBO WA HAMAS

NYOTA WA RIADHA WAREJEA NA MBWEMBWE

TIMU YA BASEBALL YAWASILI MEXICO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *