#Sports

JOBO, ST. PETERS NA KINALE WAIBUKA MABINGWA

St Joseph’s Boys Kitale walinyakua taji lao la kwanza kabisa la kitaifa katika mashindano ya Muungano wa Michezo wa Shule za Sekondari Kenya Jumamosi, baada ya fainali walioshinda 1-0 dhidi ya Musingu Boys katika uwanja wa Mumias Complex, Kakamega.

Ushindi huo uliopatikana katika dakika ya 63 ya kipindi cha pili ulipongezwa na wadau mbali mbali akiwemo Mbunge wa Kiminini Kakai Bisau ambaye alisema kuwa St Joseph’s ilionyesha kuwa Trans Nzoia sio tu kapu la chakula nchini Kenya, bali pia kitovu cha vipaji vya kipekee na ubora wa michezo.

Musingu nao waliibuka washindi wa pili katika mashindano hayo chini ya kocha Brendan Mwinamo ambaye ni mkufunzi mzoefu aliye na historia ya kufaulu katika Shule ya Upili ya Kakamega.

Wakati uo huo, St Peter’s Mumias na Kinale girls ndio washindi wa kitengo cha rugby 7s mwaka huu, katika finali zilizofanyika Kakamega.

St Peter’s walichuana na shule ya upili ya wavulana ya Koyonzo ambapo walionekana kutoshana nguvu baada ya kutoka na sare ya mabao 7 kila timu kisha St Peter’s wakawapiku Koyonzo kwa maarifa na kuongoza kwa mabao 14 kwa 12.

Kinale nao, walionekana kuwazidi maarifa wasishana wa St Joseph’s Kitale ndani ya muda wote wa mchezo ambapo waliwalaza 19 kwa 5.

Katika nafasi ya 3, Shule ya upili ya Bungoma High iliwalaza wavulana wa Bwake 7 kwa yai na kujinyakulia nafasi ya 3 huku St Theresa wakiwashinda Paul Harris 19 kwa bila na kujinyakulia nafasi ya 3 vile vile.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *