POLICE BULLETS WAINGIA NUSU FAINALI YA CAF
Mabao mawili ya Emily Moranga na Muganda Zaina Namileme yaliipa Kenya Police Bullets ushindi wa 2-0 dhidi ya wababe wa Eretria, DenDenFC na kutinga nusu-fainali ya Ligi ya Mabingwa wa CAF ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa Afrika CECAFA.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Nyayo ilishuhudia mabingwa hao wa Kenya wakipata ushindi wao wa pili mfululizo katika mchujo baada ya kuanza vyema kampeni zao kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Kampala Queens ya Uganda Alhamisi iliyopita.
Ushindi huo sasa unawaweka wasimamizi wa sheria kileleni mwa Kundi A wakiwa na alama 6, tatu mbele ya Kampala Queens huku DenDen wakisalia bila ushindi katika mechi za awali.
Kipigo hicho kinewafanya mabingwa hao wa Eritrea kupata tabu kwenye kinyang’anyiro hicho kufuatia kichapo cha 7-0 mikononi mwa Kampala Queens ya Uganda kwenye mechi ya ufunguzi.
Timu inayofundishwa na Beldine Odemba itakutana na mshindi wa Kundi C linaloundwa na JKT Queens (Tanzania), Yei Joint Stars (Sudan Kusini), JKU Princess (Zanzibar).
Nusu fainali imepangwa Septemba 14, wakati fainali itachezwa Septemba 11 lakini itatanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu Septemba 16.
Hatua ya makundi itafikia kilele Ijumaa ambapo Top G Academy ya Burundi itamenyana na CBE huku Yei FC ya Sudan Kusini ikicheza na JKT ya Tanzania.
Mechi hizo za mchujo, zitakazoendelea hadi Septemba 11, zitawakutanisha mabingwa tisa wa ligi hiyo kutoka katika kanda nzima kumenyana kuwania tiketi moja ya Fainali za Ligi ya Mabingwa wa CAF ya Wanawake nchini Misri mwezi Novemba.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































