ODM YAMTEUA MWANIAJI WA UBUNGE KASIPUL
Boyd Were, mwanawe aliyekuwa mbunge wa Kasipul Ong’ondo Were, ndiye atakayepeperusha bendera ya chama cha ODM kwenye uchaguzi mdogo eneo hilo kupata mrithi wa babake.
Hii ni baada yake kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa mchujo hapo jana kwa kura 18, 210, mpinzani wake wa karibu Newton Ogada kwa mbali akiwa na kura 3,037 huku waliosalia wakipata chini ya kura 1,000.
Matokeo hayo yalitangazwa na afisa wa usimamizi wa chaguzi za mchujo Felix Ngala mjini Oyugis.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































