SHULE KUKOSA KUTOA HUDUMA MUHIMU, KESSHA
Nyingi ya shule za umma zinakabiliwa na uhaba wa fedha huku muhula wa mwisho wa masomo ukianza, wizara ya elimu ikilaumiwa kutokana na madai ya kucheleweshwa kwa mgao wa shule hizo.
Katika traarifa, mwenyekiti wa muungano wa shule za upili KESSHA Willy Kuria, amesema shule hizo zitakosa kutoa huduma muhimu ikiwemo chakula kwa wanafunzi na maandalizi ya mitihani ya kitaifa iwapo msaada wa haraka hatutatolewa.
Shule zilizoathirika pakubwa ni zile za kutwa ambazo hutegemea mgao wa serikali kikamilifu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































