#Local News

WAKULIMA WA MIWA MAGHARIBI WAPATA AFUENI

Wakulima wa miwa katika eneo la Magharibi wamepata afueni baada ya Mahakama Kuu mjini Busia kufutilia mbali uamuzi wa kufungwa kwa muda viwanda 7 vya sukari katika ukanda huo, baada ya wakulima hao wakiongozwa na mkulima shupavu wa miwa Apostle Peter Manyuru wa kanisa la JTM, kuwasilisha kesi mahakamani.

Kupitia wakili Ruth Kimani, Wakulima wamesisitiza kuwa kuna miwa ya kutosha inayoendelea kuvunwa, na hivyo hakuna sababu ya kuzuia usagaji wa miwa na kuua sekta ya Kilimo cha miwa katika eneo la Magharibi.

Mahakama imeunga mkono msimamo wao na kubatilisha agizo la awali la bodi ya sukari kufunga kwa muda viwanda hivyo, hatua ambayo sasa imeleta matumaini mapya kwa wakulima na familia zao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAKULIMA WA MIWA MAGHARIBI WAPATA AFUENI

RAIS AZURU EMBAKASI

WAKULIMA WA MIWA MAGHARIBI WAPATA AFUENI

MBUNGE KIHARA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *