MAWAKILI WASHINIKIZA KURA YA MAONI KUHUSU NG-CDF, NGAAF
Mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2025 uliopitishwa na wabunge ili kuzijumuisha kisheria hazina za NG-CDF, ile ya uangalizi ya maseneta na NGAAF kwenye katiba umeibua ukosoaji nchini, kundi la mawakili likishinikiza marekebisho hayo kufanywa kupitia kura ya maoni.
Mawakili hao wameliandikia bunge la kitaifa na seneti kuhusu msimamo wao, wakishikilia kuwa kupitishwa kwa mswada huo ambao sasa unasubiri kuidhinishwa na maseneta, utabadili muundo wa serikali.
Wametishia kuelekea mahakamani kupinga mchakato huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































