JSC YAZUIWA KUSIKILIZA KESI YA KUMWONDOA JAJI SANKALE
Ni afueni kwa jaji wa mahakama ya rufaa Sankale Ole Kantai baada ya mahakama kuu kutoa agizo la kuizuia tume ya huduma za mahakama JSC kuendelea kusikiliza kesi inayotoka kuondolewa afisini kwa jaji huyo.
Kwenye uamuzi wake, jaji Chacha Mwita amesema vikao hivyo kuruhusiwa kuendelea ilhali kuna kesi mahakamani kuhusiana na malalamishi dhidi ya jaji huyo ambazo hazijatatuliwa kutahujumu haki yake ya kikatiba.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na seneta wa Busia na mwanaharakati Okiya Omtatah Aprili mwaka 2021, ikitaka kuondolewa kwa Ole Kantai kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya mfanyabiashara raia wa Uholanzi Tob Cohen.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































