MGOMO WA WAHADHIRI WAANZA
Shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma nchini zinatarajiwa kusambaratika kuanzia leo kufuatia mgomo wa wahadhiri ambao umenza rasmi usiku wa manane baada ya makataa yao kwa serikali kukamilika.
Katibu mkuu wa muungano wao UASU Dakta Constantine Wasonga, amesema juhudi zao kufanya mazungumzo na serikali zimefeli, mwenzake wa KUSU Charles Mukhwana, akisema hawatarejea kazini bila malalamishi yao kuangaziwa.
Hata hivyo, Waziri wa elimu Julius Ogamba, amesema juhudi zinaendelea kusitisha mgomo huo.
Imetayarishwa na Antony Ngongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































