IEBC KUANZA USAJILI WA WAPIGA KURA
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imetangaza kurejelea zoezi la kuwasajili wapiga kura wapya kuanzia Jumatatu wiki ijayo kote nchini.
Kupitia taarifa, IEBC imesema wanaolengwa ni wakenya walio na umri wa miaka 18 au Zaidi na ambao hawakuwa wamesajiliwa kama wapiga kura, na wale wanaolenga kuhamishia maelezo yao katika vituo tofuati vya kupigia kura.
Waliofuzu kusajiliwa watahitajika kuwa na vitambulisho vya kitaifa au paspoti za usafiri, huku wanaoelenga kuhamia vituo vingine wakihitajika kufika katika afisi za tume hiyo katika maeneo bunge walikosajiliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































