#Business

WAKULIMA WALINDWA DHIDI YA TABIA NCHI

Wakulima kote nchini wana kila sababu ya kutabasamu baada ya Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo kuzindua Mpango wa Bima ya Mbolea ili kuwakinga wakulima wadogo wadogo dhidi ya athari za hali ya hewa kama vile ukame na mafuriko.

Mpango huo ulizinduliwa kwa ushirikiano na shirika la Pula, Bayer, Lemonade, SOMPO Digital Lab, na Etherisc na utafanya majaribio katika kaunti 11 nchini, zikiwemo Makueni, Meru, Kisii, Kericho, na Trans Nzoia, na kufikia takriban wakulima 250,000 msimu huu.

Kila mkulima atakayeshiriki atapokea bima ya Sh7,000, sawa na mifuko miwili ya mbolea ya ruzuku. Wakulima waliosajiliwa chini ya Mfumo wa Taarifa za Kilimo Jumuishi wa Kenya (KIAMIS) wataandikishwa kiotomatiki.

Iwapo ukame, mafuriko, au hatari nyinginezo zitatokea, fidia itatolewa moja kwa moja kwenye pochi zao za rununu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

WAKULIMA WALINDWA DHIDI YA TABIA NCHI

WANARIADHA 50 KUELEKEA TOKYO JAPAN

WAKULIMA WALINDWA DHIDI YA TABIA NCHI

WAKENYA WAKIMBIA MIKOPO YA BENKI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *