#Local News

RAIS KABILA AHUKUMIWA KIFO DRC

Aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo Joseph Kabila, amehukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo baada ya kumpata na makosa ya kufadhili vita na uhaini.

Licha ya kutokuwepo mahakamani au hata kujulikana aliko, Kabila alipatikana na makosa hayo ikiwemo kufadhili kundi la waasi la M23 ambalo limeteka mashariki ya taifa hilo.

Kabila mwenye umri wa miaka 54, alichukua hatamu za uongozi kutoka kwa babake Laurent Kabila mwaka 2001 na kuongoza kwa miaka 18, kabla ya kumkabidhi Rais wa sasa Felix Tshisekedi uongozi ila wakatofautiana baadaye.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

RAIS KABILA AHUKUMIWA KIFO DRC

MAKURUTU WA POLISI KUJUA HATMA LEO

RAIS KABILA AHUKUMIWA KIFO DRC

IMBENZI APIGIA UPATO KIKOSI CHAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *