SHA KUSIMAMIA MATIBABU YA SARATANI
Ni afueni kwa wagonjwa wa saratani baada ya wizara ya afya kuanzisha mazungumzo na kampuni ya kutengeneza dawa ya Roche ili kupunguza gharama ya dawa na matibabu ya saratani kwa jumla.
Akiongea kwenye kongamano la saratani waziri wa afya Aden Duale anasema gharama hiyo itapunguzwa kutoka shilingi 120,000 kila awamu hadi shilingi 40,000 .
Duale anasema fedha hizo zitalipwa kupitia bima ya SHA na mgonjwa hatatozwa chochote.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































