KCB RFC NDIO MABINGWA WA KABEBERI 7S
Klabu ya raga ya KCB RFC imevikwa taji la kombe la Kabeberi 7s hapo jana baada ya ushindi wao wa mabao 20-10 dhidi ya Daystar Falcons katika uwanja wa RFUEA.
KCB ambao walionyesha ukakamavu wao uwanjani kwa kulinda ushindi wao, sasa wamjiongezea alama 22 na wanaongoza kwa alama 104 ambazo ni alama 9 zaidi ya wanaoshikilia nambari ya pili, Strathmore Leos.
Falcons, ambao walimaliza kipindi cha kwanza cha mchezo bila bao lolote, walionyesha kujitahidi katilka kipindi cha pili na kuambulia mabao 10 ila juhudi zao zikagonga mwamba baada ya kuzidiwa maarifa na KCB RFC.
Aidha, KCB sasa wanahitaji kufika kwenye nusu fainali ya Dala 7s ili kuvikwa taji la jumla la National Sevens Circuit crown.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































