#Sports

SHABANA FC WAANZA LIGI KWA KISHINDO

Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Shabana Peter Okidi, ameelezea kuridhishwa na ushindi wa mabao 4:2 dhidi ya limbukeni APS Bomet kwenye mechi ya ufunguzi iliyoandaliwa katika uwanja wa Gusii, akisema ni mwanzo mwema kwa msimu mpya wa 2025-26

Shabana walitawala kipindi kirefu cha mchuano huo, na kuchukua uongozi katika dakika ya 3 kupitia kwa mshambulizi wa Harambee Stars Brian Michira, ambaye alimaliza mechi hiyo akiwa na mabao 2.

Shabana watacheza mechi ya pili ya ligi dhidi ya Bandari ugani Mbaraki, Nao APS Bomet wakiwaalika Murang’a SEAL ambao walipokezwa kichapo cha bao 1:0 mikononi mwa Ulinzi Stars hapo jana.

Katika matokeo mengine, Gor Mahia walianza msimu wao kwa kichapo cha bao 1:0 dhidi ya Bidco United, AFC Leopards wakikatwa kucha kwa sare ya bao 1 dhidi ya Sofapaka.

Kariobangi Sharks waliambulia sare ya kutofungana dhidi ya Bandari, nao wanabenki wa KCB wakianza kwa kishindo walipoicharaza Tusker FC mabao 2:0 siku ya Ijumaa.

Mathare United wataanza kampeni yao dhidi ya Posta Rangers leo saa kumi alasiri.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *