#Sports

HAALAND AINGAMIZA UNITED, LIVERPOOL KILELENI

Mshambulizi wa Manchester City Erling Haaland alifunga mara 2 na kuzidisha masaibu katika klabu ya Manchester United, ambao walipokezwa kichapo cha mabao 3:0 katika mechi ya ligi kuu nchini Uingereza jana jioni.

Phil Foden alianzisha ufungaji wa mabao katika dakika ya 18 kabla ya Haaland kuingilia kati na kuwakandamiza United, ambao sasa wamepoteza mechi 3 kati ya 4 za ligi na sasa wana alama 3 pekee baada ya mechi 4 za ufunguzi.

Man U waliingia katika debi hiyo wakiwa mbele ya City kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 5, ila kibano hicho kiliiwashusha hadi katika nafasi ya 14 huku City wakipanda hadi katika nafasi ya 8 kwa alama 6, alama 6 nyuma ya vigogo Liverpool.

Kutokana na matokeo hayo, kocha mkuu wa Man United Reuben Amorin sasa amepata ushindi mara 8 pekee katika mechi 31 akiwa na United.

Liverpool wanaongoza jedwali kwa alama 12 katika mechi 4, wakifuatwa na Arsenal kwa alama 9 baada ya ushindi wa mabao 3:0 dhidi ya Nottingham Forest Jumamosi

Totenham Hostspurs wanakaa katika nafasi ya 3 kwa alama 9 vile vile, alama sawa na Bournemouth walio katika nafasi ya 4.

Chelsea waliopoteza uongozi wao dakika za jioni na kuambulia sare ya mabao 2 dhidi ya Brentford, wako katika nafasi ya 5 kwa alama 8.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HAALAND AINGAMIZA UNITED, LIVERPOOL KILELENI

KCB RFC WATAWAZWA MABINGWA WA DALA 7S,

HAALAND AINGAMIZA UNITED, LIVERPOOL KILELENI

UFICHUZI MPYA KWENYE KESI YA REX

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *