MWANZO WA UFUNGUZI WA MWISHO
Wanafunzi wa shule za msingi na upili kote nchini wamerejelea muhula wa tatu na wa mwisho ambao umeratibiwa kuwa mfupi na muhimu zaidi, ukianza hii leo hadi mwishoni mwa mwezi Oktoba kabla ya mitihani ya kitaifa.
Wengi wa wazazi wamelalamikia kupanda kwa gharama ya vitabu vya wanafunzi na ada za usafiri, wakiitaka serikali kudhibiti uuzaji wa vitabu na sekta ya uchukuzi ili kuwalinda dhidi ya ongezeko hilo.
Mapema leo, msongamano wa magari umeshuhudiwa katika barabara za miji kadhaa, wanafunzi wanaporejea shuleni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































