#Local News

MBADI, OPARANYA WAKABILIWA NA FAINI

Mawaziri Wycliffe Oparanya wa biashara ndogo ndogo na mashirika na mwenzake wa fedha John Mbadi, wameagizwa kufika mbele ya kamati ya leba na masuala ya kijamii katika bunge la seneti hii leo baada yao kukosa kufanya hivyo hapo jana.

Oparanya ambaye ametakiwa kutoa maelezo kuhusu malipo ya kuachishwa kazi kwa wafanyakazi wa zamani wa shirika la KCC, amekosa kufika mbele ya kamati hiyo mara 7 sasa, akiagizwa kfika hii leo au awasilishe stakabadhi hitajika.

Kulingana na agizo la seneti, wawili hao watatozwa faini isiyopungua shilingi elfu 500 iwapo watakosa kufika mbele ya kamati hiyo.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MBADI, OPARANYA WAKABILIWA NA FAINI

WAKENYA WAHEPA MIKOPO- RIPOTI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *