#Local News

RUTO, WAKUU WA WALIMU IKULU

Viongozi wa miungano ya walimu nchini wameratibiwa kufanya kikao na Rais William Ruto hii leo katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watapata fursa ya kuwasilisha malalamishi yao kwa rais moja kwa moja ikiwemo kucheleweshwa kwa mgao wa shule.

Viongozi hao wamekariri kuwa mkutano huo utajikita kujadili matatizo yao kama vile suala la kupandishwa vyeo kwa walimu na uajiri wa walimu wanagenzi, na wala si siasa jinsi inavyofasiriwa na baadhi ya wakenya.

Miongoni mwa miungano iliyoalikwa ni KNUT, KUPPET, na usimamizi wa walimu wakuu wa shule za msingi na upili, taarifa zikisema rais atatumia kikao hicho kuelewa kwa kina changamoto katika sekta ya elimu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

RUTO, WAKUU WA WALIMU IKULU

BODA WAANGUKIWA NA MASHARTI MAGUMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *