#Local News

SERIKALI YA KIRINYAGA YATANGAZA AFUENI YA FIGO

Shughuli za matibabu katika hospitali ya Kerugoya kaunti ya Kirinyaga zinatarajiwa kurejelea hali ya kawaida baada ya kutatizika kutokana na kufeli kwa mashine za kuosha figo na kuwaacha wagonjwa taabani.

Hii ni baada ya serikali ya kaunti hiyo kutangaza kwamba itaweka mashine mpya 25 katika hospitali hiyo na hospitali nyingine za kaunti hiyo, ikiwemo Sagana, Kimbimbi na Kianyaga ambayo itasaidia katika matibabu ya figo.
kulingana na gavana Anne Waiguru mashine 10 zitawekwa katika
hospitali ya kaunti ya Kerugoya, huku zilizosalia zikigawanywa kwa hospitali nyingine.

Hatua ya serikali hiyo inajiri baada ya wagonjwa wa figo kukosa matibabu kufuatia kufeli kwa mashine 6 kati ya 8 zilizokuwa kwenye hospitali ya Kerugoya ambayo ni hospitali
ya pekee ya umma ya matibabu ya figo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SERIKALI YA KIRINYAGA YATANGAZA AFUENI YA FIGO

CAPEVERDE WALAZA CAMEROON

SERIKALI YA KIRINYAGA YATANGAZA AFUENI YA FIGO

MASOMO YA VYUO VYA UMMA PEMBAMBA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *