#Sports

HOWE AELEKEZA NGUVU ZAKE KWA WACHEZAJI WAPYA

Meneja wa Newcastle Eddie Howe ametangaza kuwa anaelekeza nguvu zake kwa wachezaji wanaotaka kuchezea Newcastle baada ya bao la ushindi dakika ya 100 kutoka kwa mchezaji wa akiba Rio Ngumoha, kuipa Liverpool ushindi muhimu. Kipigo hicho kilikuja huku kukiwa na hali ya taharuki inayomzunguka mshambuliaji nyota Alexander Isak, ambaye inasemekana anajaribu kulazimisha kuhamia Liverpool na anafanya mazoezi tofauti na kikosi hicho. Timu ya wachezaji kumi ya Howe ilikuwa imeonyesha ari kubwa ya kupambana na kurejea 2-2 baada ya kadi nyekundu ya Anthony Gordon kipindi cha kwanza, lakini wakanyimwa pointi moja katika dakika za mwisho baada ya bao hilo la Ngumoha ambaye aliweka recodi ya kuwa mchezaji wa nne mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kufunga kwenye ligi kuu ya uingereza.

Imetayarishwa na Nelson Andati.

HOWE AELEKEZA NGUVU ZAKE KWA WACHEZAJI WAPYA

CHAN YAINGIA NUSU FAINALI

HOWE AELEKEZA NGUVU ZAKE KWA WACHEZAJI WAPYA

TETESI ZA UHAMISHO ZA LIGI YA PREMIA 

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *