GAVANA BARASA ACHAGULIWA KUONGOZA ODM KAKAMEGA
Gavana wa Kakamega Fernandez Barasa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la Kakamega kufuatia uchaguzi wa mashinani wa chama hicho hapo jana.
Barasa alitangazwa kuwa mshindi baada ya mrengo unaoongozwa na mbunge wa Lugari Nabii Nabwera na mwakilishi wa kike Elsie Muhanda kuondoka katika kituo cha kupigia kura, baada ya pendekezo lao la kutaka kura ifanywe kwa njia ya siri kukataliwa.
Hata hivyo akiwahutubia wanahabari baadaye, Nabwera alijitangaza kuwa mwneyekiti.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































