#Local News

UTATA WAENDELEA KUZINGIRA MGAO WA SHULE

Kauli kinzani kutoka kwa Wizara ya Elimu na Hazina ya Kitaifa zimezua sintofahamu kuhusu hali ya utoaji wa fedha kwa ajili ya shule za umma, na kuibua wasiwasi kuhusu ucheleweshaji wa fedha na athari zake katika uendeshaji wa shule.

Katibu Mkuu wa Elimu ya Msingi Julius Bitok amesema kwamba shule za umma zilipokea asilimia 60 pekee ya mgao wao wa masomo, huku serikali ikijitahidi kutoa salio lililosalia kabla ya mwisho wa muhula.

Hata hivyo, kauli ya Bitok inakinzana na ya awali ya Katibu Mkuu wa Hazina ya kitaifa Chris Kiptoo, ambaye mnamo Mei alisisitiza kuwa serikali ilikuwa imetoa pesa zote za matumizi ya mwaka wa kifedha wa 2024/25.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, serikali ilitenga Sh54.6 bilioni kwa Elimu ya Sekondari ya Kutwa Bila Malipo, Sh30.4 bilioni kwa Shule za Sekondari za wavulana, na Sh8.4 bilioni kwa Elimu ya Msingi Bila Malipo katika mwaka huu wa fedha.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

UTATA WAENDELEA KUZINGIRA MGAO WA SHULE

TSC KUWAPA WALIMU MAFUNZO YA CBE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *