#Sports

MARTINELI AIOKOLEA ARSENAL ALAMA, MAN U WAANGUKA NA CHELSEA

Bao la Gabriel Martinelli lilifufua matumaini ya Arsenal kupigania taji la ligi kuu ya Uingereza EPL baada ya kuwahakikishia sare ya bao 1 nyumbani Emirates dhidi ya Manchester City.

City walikosa adabu ya mgeni kunako dakika 9 baada ya mshambulizi wao Erling Haaland kuwaweka kifua mbele kutokana na shambulizi la kushtukiza alilolianzisha katikati ya uwanja na kisha kumegewa pasi na kiungo Tijjani Reijnders.

Hata hivyo, Martinelli aliyeingia kama nguvu mpya, aliiokolea Arsenal alama moja katika dakika za lala salama licha ya City kuweka ukuta ili kulinda uongozi wao.

Sare hiyo ni ushindi kwa Liverpool ambao sasa wako alama 5 mbele ya Arsenal walio katika nafasi ya pili, na alama 8 mbele ya City ambao sasa wameshuka hadi nafasi ya 9.

Liverpool wameshinda mech izote 5 za mwanzo wa ligi, baada ya ushindi wa magoli 2:1 dhidi ya Everton wikendi.

Katika matokeo mengine ya wikendi, Manchester United walioyesha dalili za kuimarika baada ya kuanguka na Chelsea, katika mechi iliyoshuhudia kadi 2 nyekundi kwa wachezaji Robert Sanchez na Casemiro.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MARTINELI AIOKOLEA ARSENAL ALAMA, MAN U WAANGUKA NA CHELSEA

SHABANA FC WAANZA LIGI KWA KISHINDO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *