WAHUDUMU WA UHC WAPATA AFUENI
Hatimaye mustakabali wa wahudumu wa afya walio chini ya mpango wa afya ya wote UHC umepata suluhu baada ya serikali kuu kusitisha zoezi la kuwahamishia kwa serikali za kaunti na badala yake kukubali kuwalipa mishahara yao kulingana na viwango vya tume ya SRC kwa mwaka mmoja ujao.
Makubaliano hayo yalijiri kufuatia mazungumzo ya dakika za mwisho baina ya serikali kuu na baraza la magavana, na kumaliza vuta nikuvute iliyokuwa imewaweka wahudumu hao katika njia panda.
Aidha, serikali imekubali kutoa malipo ya SHA kwa hospitali za umma zilizo chini ya kaunti kufikia kila tarehe 14.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































