#Business

WAKENYA WAHEPA MIKOPO- RIPOTI

Zaidi ya theluthi mbili ya Wakenya wameachana na mpango wa kuchukua mikopo mipya mwaka huu, hasa kutokana na gharama kubwa za kukopa. Utafiti uliofanywa na TransUnion unaonyesha kuwa 68% ya watu wazima wameahirisha mipango ya kutuma maombi ya mikopo.

Kama ilivyoripotiwa, gharama kubwa za kukopa zinasalia kuwa sababu kuu, iliyotajwa huku asilimia 42 ya waliohojiwa ambalo ni ongezeko kutoka asilimia 41 ya waliohojiwa mwaka uliopita. Matatizo mengine ni pamoja na kupata ufadhili mbadala na hofu ya kukataliwa kutokana na kipato au hali ya ajira.

Hali hiyo inaendelea licha ya Kiwango cha Benki Kuu (CBR) kushuka kutoka 13% hadi 10% katika mwaka uliopita. Hata hivyo, wastani wa viwango vya mikopo vimepungua kidogo tu, kutoka 16.6% hadi 15.65%, kuonyesha marekebisho ya polepole na benki za biashara.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

WAKENYA WAHEPA MIKOPO- RIPOTI

MBADI, OPARANYA WAKABILIWA NA FAINI

WAKENYA WAHEPA MIKOPO- RIPOTI

SERIKALI YAAPA KUMWAJIBISHA GACHAGUA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *