MOI, WAHADHIRI WAKOSA MWAFAKA
Huenda shughuli za masomo zikaendelea kutatizika katika chuo kikuu cha Moi masomo yanaporejelewa, baada ya wahadhiri chuoni humo kukatalia mbali pendekezo la usimamizi wa chuo hicho kumaliza mgomo wakisema kwamba pendekezo hilo halijaafikia malalamishi yao.
Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano wa UASU tawi la Eldoret Busolo Wekesa, wahadhiri hao wamesema licha ya mazungumzo na chuo hicho kuanzia wiki jana, wamekosa kuafikiana kuhusu mgao uliotolewa walioutaja kuwa mdogo zaidi.
Wanashinikiza kulipwa mishahara ya mwezi Juni na Julai mwaka huu kulingana na makubaliano baina yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































