SERIKALI YAAPA KUMWAJIBISHA GACHAGUA
Serikali imewatahadharisha wakenya dhidi ya kuhudhuria mikusanyiko ya kumkaribisha nyumbani kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua atakaporejea nchini hii leo kutoka Marekani iwapo mikusanyiko hiyo hatitakuwa na kibali.
Katika kikao na wanahabari, waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen na inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja, wamesema serikali haitaruhusu vikao vya kutatiza amani na biashara kufanyika nchini.
Gachagua anayerejea leo baada ya ziara ya wiki 6, ameratibiwa kufanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kamukunji mtaani Shauri Moyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































