IEBC YAPINGA MADAI YA WIZI WA KURA
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Erastus Ethekon, amelihakikishia taifa kuwa uchaguzi wa mwaka 2027 utakuwa wa huru, wazi na haki na kwamba hapatakuwa na mwanya wa wizi wa kura jinsi inavyodaiwa na baadhi ya wandani wa Rais William Ruto.
Katika kikao na wanahabari, Ethekon amesisitiza kuwa tume hiyo ni huru, na haitatekeleza majukumu yake nje ya sheria za uchaguzi na katiba ya Kenya.
Hakikisho lake linajiri huku baadhi ya viongozi wa Kenya Kwanza wakitishia kufanya kila wawezalo ili kumhakikisha Rais Ruto muhula wa pili madarakani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































