LIVERPOOL WAKUBALI KUMSAJILI HUGO
Liverpool wamekubali kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Hugo Ekitike kwa mkataba wa awali wa pauni 69 kulingana na ripoti.
Mabingwa hao wa Premier League walielekeza nguvu zao kwa Ekitike kufuatia Newcastle kukataa kumuuza mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 150 na Magpies.
Newcastle na Manchester United pia walikuwa na nia ya kumnunua Ekitike, lakini Liverpool wanaonekana kuwa tayari kushinda katika kinyang’anyiro cha kuwania mmoja wa nyota wachanga wa Uropa. Inaaminika Reds wamekubali kulipa pauni milioni 10 zaidi za nyongeza ili kumsajili Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye bei yake ya jumla inaweza kufikia pauni milioni 79.
Mara tu uhamisho utakapokamilika, Ekitike ataungana na kikosi cha Arne Slot kwenye ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya barani Asia.
Ekitike alifunga mabao 22 katika michezo 48 katika mashindano yote akiwa na Frankfurt msimu uliopita baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga akitokea Paris Saint-Germain.
Alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika wakati wa mechi ya kirafiki ya timu yake ya kabla ya msimu mpya dhidi ya FSV Frankfurt siku ya Jumamosi, huku bosi wa Eintracht Dino Toppmoller akikiri kwamba kuondoka kwa Ekitike kulikuwa “hasara mbaya”.
The Reds pia wanaaminika kuwa tayari kumuuza mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, huku fowadi wa Colombia Luis Diaz akilengwa na ofa iliyokataliwa kutoka kwa Bayern Munich.
Liverpool tayari wametumia pauni milioni 116 kumnunua mchezaji wa Ujerumani Florian Wirtz, pamoja na kuwasajili mabeki Jeremie Frimpong na Milos Kerkez kutoka Bayer Leverkusen na Bournemouth mtawalia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































