MKENYA STEPHEN MUNYAKHO SASA YUKO HURU
Mkenya Stephen Munyakho aliyehukumiwa kifo huko Saudia Arabia sasa yuko huru na anatarajiwa kurejea nchini.
Haya ni kwa mujibu wa katibu katika wizara ya masuala ya kigeni Korir Sing’oei anayesema watatoa taarifa zaidi kuhusu mipango na siku atakaporejea nchini.
Munyakho ambaye sasa anajulikana kama Abdul kareem alipewa hukumu hiyo baada ya kupigana na mwenzake raia wa Yemen wakiwa kazini mwaka wa 2011 na kisha majeraha aliyopata raia huyo kupelekea kifo chake.
Imetayarishwa na Maureen Mukhobe
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































