#Local News

WAHADHIRI MOI WAENDELEA NA MGOMO

Mgomo wa wahadhiri katika Chuo Kikuu cha Moi umeingia wiki ya tatu, huku muunganio wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu (UASU) na usimamizi wa chuo hicho wakikosa kuelewana.

Naibu Chansela wa chou hicho, Profesa Kiplagat Kotut, ametoa hakikisho kuwa mgomo utapata suluhu, akisema mazungumzo mapya yanapangwa ili kushughulikia masuala yaliyowasilishwa na muungano.

Hata hivyo, mazungumzo yaliyofanyika wiki iliyopita kati ya pande hizo mbili yalimalizika bila makubaliano huku maafisa wa UASU wakisistiza kuwa hawatarejea kufundisha hadi matakwa yao yote yatakapotekelezwa

Haya yanajiri huku wahadhiri hao wakiibua madai kwamba wanatishiwa kufutwa kazi iwapo wataendelea na mgomo huo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAHADHIRI MOI WAENDELEA NA MGOMO

WAKUU WA MBUGA YA NAKURU MAHAKAMANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *